Friday, 17 March 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wandishi wa habari Mkoani Dodoma leo Machi 17, 2017 kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana Machi 16, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwa sababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. (PICHA NA IKULU)


Reactions:

0 comments:

Post a Comment