Friday, 3 March 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi, Machi 3, 2017.(PICHA NA IKULU).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi minne na si vinginevyo.RAIS John Pombe Magufuli, ameagiza vyombo vya dola kuwanyang’anya pasi za kusafiria (Passport), makandarasi wa kampuni moja ya India, wanaotekeleza mradi wa maji wa Ng’apa ulioko mkoani Lindi.
Rais ameyasema hayo jioni hii Machi 3, 2017, wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Lindi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea mikoa ya Kusini.
“Tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimewanyang’anya pasi zao za kusafiria ili wasitoke hapa Lindi, wabaki huko huko Ng’apa wakifanya kazi.” Alisema Rais Magufuli na kushangiliwa na umati wa watu.
“Nilichogundua wakati nilipokwenda kukagua mradi huo nimegundua kuwa hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika, hata Waziri na maafisa wake hawakupenda niende kukagua mradi huo, lakini mimi niliwaambia naenda kukagua mradi wa Ng’apa.” Alisema na kuongeza.
“Makandarasi hawa kutoka India, walipogundua kuwa ninakuja Lindi, wakaenda na kuwafisha kofia ngumu wafanyakazi, wakajifanya wako kazimi lakini ukiangalia hakuna kilichokuwa kikifanyika hata ndondo nazo zilianza kupata kutu.” Alisema Rais.
Aidha kufuatia mkwamo huo Rais ametoa miezi minne mradi huo uwe umekamilika kwani hakuna kisingizio chochote cha ukosefu wa fedha.
“Titawaomba hawa walioahidi kufadhili mradi huu, kama hawawezi kutupatia fedha hizo, sisi serikali tutazitoa.” Alisisitiza.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment