Thursday, 30 March 2017MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo Machi 30, 2017, imetengua hukumu ya mahakama ya chini Wilayani Kilombero, aliyopewa Mbunge wa Kilombero wa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Lijualikali na kumuachia huru.
Mahakama hiyo ya chini ya Kilombero, ilimuhukumu kifungo cha miezi 6 jela.  
January 11, 2017 Mbunge wa Kilombero kwa ticket ya CHADEMA Mhe.Peter Lijualikali alihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa  kupatikana na kosa la kufanya vurugu wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na kushitakiwa kwa  kuwashambulia polisi siku hiyo ya uchaguzi, huku aliyekuwa dereva wake, Stephano Mgatta akihukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita..
Uamuzi wa mahakama kutengua hukumu hiyo umekuja baada ya kukuta Lijualikali hana kosa na hivyo kutengua hukumu iliyotolewa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Kilombero, Morogoro.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment