Saturday, 11 March 2017


NA K-VIS BLOG
NYUMBA kadhaa zilizojengwa ndani ya mita 30 kutoka reli ya kati eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam, zimebomolewa mapema leo alfajiri Machi 11, 2017.
Mashuhuda wanasema, mapema alfajiri tingatinga likisimamiwa na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia, walifanya zoezi hilo la kubomoa nyumba hizo huku wenye nyumba na wapangaji wakihami mali zao.
Taarifa zinasema wenye nyumba hizo waliwekewa alama za X zikimaanisha nyumba hizo hazikustahili kujengwa kwenye eneo hilo na kwamba wamiliki wake walitakiwa kuzibomoa.
Pichani ni jinsi zoezi hilo lilivyokuwa likiendela.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment