Wednesday, 8 March 2017


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitembea sehemu ya ukaguzi wa mizigo bandari ya Zanzibar, Machi 8, 2017. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa dawa za kulevya huku akiliagiza jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na uongozi wa bandari, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza  nguvu kazi ya Taifa

 Winchi ikinyanyua mizigo kwenye bandari hiyo

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa dawa za kulevya huku akiliagiza jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na uongozi wa bandari, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza  nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu bandariya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma. (Pichana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

 Eneo la kupokelea mizigo
Naibu Waziri Masauni akiangalia mifumo ya komputa inayotumika kufanyia ukaguzi wa mizigo
Reactions:

0 comments:

Post a Comment