Friday, 17 March 2017


KAMPALA, UGANDA
Msaidizzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, (AIGP), ambaye pia ni Msemaji wa jeshi hilo, Andrew Felix Kaweesi ameuawa kwa kupigwa risasi mita chache, kutoka nyumbani kwake mapema saa 3:30 asubuhi Machi 17, 2017.
 Katika mauaji hayo walinzi wake wawil, (bodyguards), mmoja kitambuliwa kama Godfrey Mambewo, pia waliuawa.Taarifa za vyombo vya habari zinasema, kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Taarifa zaidi zinaema Kaweesi alikuwa anatarajiwa kuhutubia wanafunzi wa UCU, leo Ijumaa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment