Thursday, 16 March 2017JUHUDI za Waziri wa Mmabo ya Ndani ya Nchi, na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, Mwigulu Lameck Nchemba,(pichani chini) “amempeleka” aliyekuwa kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm, kuifundisha Singida United iliyopanda daraja mwaka huu na sasa itacheza ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Taarifa zinasema Mwigulu ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya timu hiyo, amemwachia jukumu Mholanzi huyo kufanya usajili na tayari ameanza kwa kumsajili
kiungo Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn FC ya Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili.(pichani kocha mpya wa Singida United, Mdachi Hans Van der Pluijm, akimkabidhi jezi mchezi mpya wa timu hiyo, Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu. PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY SPORTS ONLINE)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment