Friday, 10 March 2017


MVUA iliyoambatana na upepo mkali imeezua mapaa ya nyumba zinazokadiriwa kufikia 153 ikiwemo shule ya msingi Muungano kwenye kata ya Mnazi Mmoja na Mingoyo mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, 

Shaibu Demanga, amesema takriban kaya 260 ikiwemo miundombinu ya Shule ya Msingi Muungano imeharibiwa vibaya.
Taarifa zinasema Mvua hiyo iliyonyesha majira ya jioni Machi 9, 2017 imeleta madhara makubwa ingawa viongozi wa shule ya msingi Muungano wamesema, madarasa 4 na nyumba 1  ya mwalimu zimeezuliwa  lakini haitafungwa na badala yake wanafunzi wataendelea na masomo yao.
Tathimini inaendelea mpaka sasa shule ya msingi muungano pamoja na hizo  kuna jumla ya nyumba 153 za wakazi zimeharibiwa mvua hizo.
Taarifa zinasema sio tu nyumba zilizoharibika bali pia mvua hiyo ya upepo imeangusha miti na kuharibu miundombinu mingine.

 Moja ya majengo ya shule ya msingi Muungano baada ya kuezuliwa na upepo huo


Reactions:

0 comments:

Post a Comment