Wednesday, 29 March 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, (pichani kushoto), amehojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa muda wa zaidi kidogo ya masaa matatu mjini Dodoma Machi 27, 2017.
Makonda ambaye alifika  amefika mbele ya kamati hiyo kufuatia wito wa Kamati  kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi Februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa  Februari 8, 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexander Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment