Friday, 10 March 2017NA K-VIS BLOG, DODOMA
MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi CCM, yamefikia pazuri ambapo Machi 12, 2017 Halmashauri Kuu ya Chama hicho kinachotawala, itakutana na hatimaye Machi 12, Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho utafanyika kwa lengo la kufanyia marekebisho katiba yake ya mwaka 1977.
Leo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Rorick Mpogolo na Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, na Uenezi, Humphrey Polepole walifanya ukaguzi wa mwisho mwisho wa ukumbi utakaotumika kufanyia mkutano huo. Ukumbi huo ni ule wa Mikutano ya Kimataifa unaomilikiwa na chama hicho ulioko nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.

 Hapa ndipo utakapofanyika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM mjini Dodoma Machi 12-13, 2017

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi,   Humphrey Polepole akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jitegee, Antony Machunde walipokuwa wakikagua ukumbi wa Mkutanao Mkuu maalum wa CCM, utakaoanza mwishononi mwa wiki.

Naibu katibu Mkuu CCM (Bara), Rodrick Mpogolo akimsikiliza Katibu Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole walipokuwa wakipanga mikakati kufanikisha mkutano mkuu wa CCM uatakaofanyika katika ukumbi wa mikutano, Dodoma leo Machi 10, 2017
Reactions:

0 comments:

Post a Comment