Sunday, 26 March 2017

sau1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.
sau2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasikwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
sau3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji.
sau4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi. Gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 60 ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Mkuu wa Gereza hilona kuhudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo vilivyo chini ya wizara yake pamoja na viongozi wa wilaya hiyo. 
sau5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza hilo. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment