Tuesday, 14 March 2017

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya kukagua sehemu zilizokumbwa na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wale wote waliojenga mabondeni kuhama mara moja kwani wengi wao walikwishapatiwa viwanja kule Mabwepande nje kidogo ya jiji.
Makonda alisema, watu hao ni watu wabaya kwani walipewa viwanja Mambwepande, na wako katika makundi mawili, wapo ambao wamehama na kuwapangisha watu kwa bei nafuu na wengine wameuza viwanja walivyopewa na kurejea huko mabondeni. "Natoa wito, wote wanaoishi kwenye maeneo haya hatarishi wahame mara moja na kurejea kwenye maeneo yao salama." Alisisitiza.
Tayari Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewaagiza Makamanda wa polisi wa wilaya kuhakikisha wale wote wanaoishi kwenye maeneo ya mabondeni wanawaondoa kwa nguvu.
"Jeshi la polisi kazi yake ni kulinda mali na usalama wa wananchi na sisi hatuwezi kukubali kuona watu wanaishi kwenye maeneo ambayo yatahatarisha maisha yao kwa hivyo kama wananisikia wahame mapema kabla mkono wa sheria haujawafikia." Alisema Kamanda Sirro wakati wa taarifa yake ya kila siku kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Macvhi 14, 2017.
amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.
Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2017 ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko ya mvua zilizonyesha Machi 13, 2017.
"kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua hizi zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50, maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba "Amesema Makonda
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mt Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha Dar es Salaam na kuleta madhara kwa wakazi hao
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuza maembe. (Na Mtaakwamtaa blog)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment