Tuesday, 14 March 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo amezindua mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.
Mama Samia  amesisitiza kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo na matumizi sahihi ya vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuinua kiwango cha Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini
Aidha Makamu wa Rais amepongeza jitihada na ubunifu wa Mbunge wa Jimbo hilo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Ndg Anthony  Mavunde na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuwahudumia wanadodoma Mjini.
Pamoja na hilo Mama Samia ameahidi kuunganisha Jimbo la Dodoma Mjini na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia watoto wa kike kupitia mfumo wa ufundishaji kidigitali wa Sillicon Valley.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Pro Futuro, Rosemary Terry (kushoto) juu ya Vishikwambi (Ipad) vitakavyotumika katika kufundishia shule 10 zilizopo ndani ya jimbo la Dodoma mjini, kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
 Makamu wa Rais Mama Samia  Suluhu Hassan (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wageni waalikwa wengie wa meza kuu wakionesha baadhi ya Vishwambi mara baada ya kuuzindua mpango huo wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini. 
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla fupi uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.
 Baadhi ya Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini tukio hilo
 Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo adhimu kwao
Reactions:

0 comments:

Post a Comment