Monday, 27 March 2017


Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo Machi 27, 2017. Katika ziara aliyoifanya nchini mwishoni  mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madheebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa wagonjwa. Timu ya  wataalam hao ambao idadi yao ni sita  imeshawasili nchini na tayari wameanza kufanya upasuaji ambao utachukuwa  siku tano na wanatarajia kufanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba  ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) na upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo inamatatizo na inahitaji kubadilishwa kwa wagonjwa 15.(PICHA NA ANNA NKINDA-JKCI)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment