Friday, 10 March 2017

 Mbunge wa Arusha Mjini, (CHADEMA), Godbles Lema, (kushoto),akiwa na Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara leo Machi 10, 2017 jijini Arusha tangu aachiliwe kwa dhamana kufuatia kesi ya uchochezi inayomkabili.
Lema ambaye alipewa dhamana mapema wiki hii baada ya kukaa rumande kwa muda mrefu, alisema, ataendelea kutetea demokrasia bila woga, kauli ambayo iliungwa mkono na Wema Sepetu ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu, ambaye naye alisema, yuko bega kwa bega na Lema katika kutetea demokrasia ya nchi.
 Lema akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha huko Ngarenaro
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano huo


Reactions:

0 comments:

Post a Comment