Monday, 13 March 2017


NA K-VIS BLOG
RAIS John Pombe Magufuli amesema atakutana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili kujadili njia bora za kuondoa kero zao zinazowakabili.
Rais aliyasema hayo leo asubuhi wakati akiongea moja kwa moja kwenye kipindi cha Clouds 360, ambapo mgeni alikuwa msanii Nasibu Abass, almaarufu kama Diamond Platnamz
Rais Magufuli, alipiga simu baada ya kusikia malalamiko ya Diamond Platnamuz aliyesema, kuwa wasanii wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuibiwa nyimbo zao au kulipwa malipo madogo na kampuni za simu.
“Ninaomba mheshimiwa Rais, aagize vyombo vyake vituwekee ulinzi kwenye mtandao wetu, ili tuweze kupata kipato zaidi na kuweza kulipa kodi za serikali.”Alisema Diamond
“Nimesikia Diamond maombi yake na nimeyapokea, nimemfurahia kwamba yeye ni CCM na nimefurahi kuwa hivi sasa ana watoto wawili, wakati wa kampeni alikuwa na motto mmoja, hongera sana Doamond.” Alisema Rais Magufuli, ambaye amekuwa mpenzi mkubwa wa kipindi cha Clouds 360.
“Tutapanga siku moja nikutane nao ili tuangalie namna nzuri ya kuwasaidia, nawashukuru sana nawatakia kipindi chema, ujue nawaangalia hapa live, na hongera sana Diamond

Rais John Magufuli
Reactions:

0 comments:

Post a Comment