Thursday, 16 March 2017MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,leo Machi 16, 2017, imetupiliaa mbali kesi ya Kikatiba ya kulalamikia Kanuni za Chama cha Mawakili Tanganyika,( TLS), iliyokuwa imefunguliwa na wakili Onesmo Mpenzile dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali .
Uamuzi huo umesomwa na Jaji Ignus Kitutu ambaye amesema mahakama imeamua kuitupilia mbali shauri hilo kwasababu imebaini hati ya kiapo ina dosari za kisheria pia mlalamikaji alipaswa afungue ombi la marejeo (Judicial Review) mahakamani na siyo kama alivyofanya.
Wakati huo huo taarifa kutoka Dodoma nazo zinasema Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma nayo ifuta rasmi kesi iliyofunguliwa na Wakili Godfrey Wasonga kupinga uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha wiki hii.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment