Saturday, 18 March 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 18, 2017.Serikali imetangaza ajira ya madaktari 500 ambao hawako kwenye ajira ya utumishi wa Umma ili waende Kenya kufanya kazi, baada ya serikali ya nchi hiyo kuiomba Tanzania iokoe jahazi kufuatia mgomo wa muda mrefu wa madaktari nchini Kenya. (PICHA NA IKULU)Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba ambaye aliambatana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kabla hawajaondoka Ikulu jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini,(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali. (PICHA NA IKULU)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyeambatana  pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment