Monday, 20 March 2017


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,(pichani juu), ameipa saa 24 kamati aliyoiunda kuchunguza “kashfa” ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, “kuvamia” Ofisi za Clouds Media Group, (CMG), Alhamisi usiku akiwa na askari wenye silaha.

Akizunguzma wakati wa ziara yake mapema leo Machi 20, 2017 kutembelea studio za Clouds Mikocheni B jijini Dar es Salaam, ili kutoa pole kufuatia tukio hilo linalolaaniwa na tasnia ya wanahabari na watu wenye kupendelea uhuru wa vyombo vya habari kote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwa na askari wapatao sita wenye silaha za moto, (bunduki), “walivamia” Ofisi za Clouds Ijumaa usiku kwa lengo la kuhoji ni kwanini kipindi cha mwanamama anayedaiwa kuzaa na Askofu Josephat Gwajima, haikurushwa hewani.
Uongozi wa Clouds alisema haukurusha kipindi hicho kwa vile kinakiuka maadili na hakikuwa kimekamilika kwa mtuhumiw akupata nafasi ya kuzungumza.
 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment