Thursday, 30 March 2017


Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akitoa ufafanuzi  kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara yake kwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyesimama akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, huku  Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wake,  Balozi  Hassan Simba Yahaya wakimsikiliza kwa makini.  Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Balozi  Hassan Simba Yahaya anayemfuatia wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini [IGP] Ernest  Mangu aliyesimama  kuhusu Oparesheni mbalimbali za kuzuia uhalifu hapa nchini, wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, akiwa pamoja na watendaji wengine wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, akimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi  Adad Rajab wakati Mwenyekiti huyo hayupo pichani, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kuipitia Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bjeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment