Sunday, 12 March 2017NA K-VIS BLOG, DODOMA
MWENYEKITI wa CCM, Rais John Pombe Magufuli ameonya wale wote waliojipanga kuvuruga mkutano mkuu maalum wa chama hicho unaoendelea mjini Dodoma leo Machi 12, 2017, kuwa watakumbana na mkono wa sheria na kuwaonya wasithubutu kufanya hovyo kwani hatua za kisheria na kimaadili zitachukuliwa dhidi yao.
Dkt. Magufuli aliyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano mkuu maalum wa chama hicho unaoendelea hivi sasa.
Mwenyekiti huyo wa CCM pia ameupa jina ukumbi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Dodoma kinachomilikiwa na CCM kuwa ukumbi wa KIKWETE, (KIKWETE Hall), ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM ambaye ndiye aliyewezesha ujenzi wa ukumbi huo.
“Kabla sijaanza hotuba yangu, ndugu Kikwete yuko hapa, ngoja aje kwanza ndugu Kikwete kabla sijaendelea na hotuba yangu nianze kwa kueleza kuwa tuko kwenye ukumbi mzuri sana na mmoja wa waliofanikisha kuwa na ukumbi huu ni ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kwa hivyo napendekeza ukumbi huu uitwe Kikwete hall.” Alisema Dkt. Magufuli na kuwahoji wajumbe juu ya pendekezo hilo ambao wote waliitikia kuunga mmono pendekezo hilo.
“Kwa hivyo natangaza kuanzia leo hii, ukumbi huu utaitwa Kikwete Hall.” Alisema.Reactions:

0 comments:

Post a Comment