Sunday, 26 March 2017Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,  Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na wanahabari kuhusu Jeshi hilo kuanza kulipa deni wanalodaiwa na Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanzia Machi 28. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Ngome jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2017.

NA K-VIS BLOG
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, amesema JWT itapunguza deni lake la umeme inalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kuanzia Machi 27, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya JWTZ, Ngome Upanga jijini Dar es Salaam, leo Machi 26, 2017, Mkuu huyo wa Majesho alisema, “tayari nimeshaagiza idara husika kuandika hundi na kuiepeleka TANESCO Machi 27, 2017 ili kupunguza deni tunalodaiwa na Shirika letu la umeme linalozidi kidogo Shilingi Bilioni 3.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Mkuu huyo wa Majeshi alisema, “Natoa wito kwa taasisi nyingine kulipa madeni ya TANESCO ili tuliwezeshe shirika letu liwe na uwezo wa kutoa huduma kwa uhakika na hivyo kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata umeme.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Rais John Pombe Magufuli, akizindua ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Mtwara cha umeme wa 133Kv, aliagiza Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kukata umeme kwa wadaiwa sugu. “Hata kama Ikulu wanadaiwa umeme, kata, hata Jeshi, polisi na kwingineko, wewe kata.” Alisagiza Rais Magufuli.
Baada ya agizo hilo la Rais, uongozi wa Shirika hilo uliitisha waandishi wanhabari na kutoa siku 14 kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao  vinginevyo huduma ya umeme ingesitishwa baada ya muda huo.
JWTZ, inakuwa taasisi ya kwanza nyeti kutoka hadharani na kuahidi kupunguza deni hilo la umeme, tayari Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), nalo limeahidi kupunguza deni la umeme.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment