Saturday, 11 March 2017


MBUNGE wa Nzega mjini Hussein Bashe, amesema Katibu Mkuu wa CCM, ndiye atakayezungumzia nini kiliwatokea yeye na wenzake, Joseph Kasheku almaarufu kama Msukuma na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Mkuranga.
Bashe na wenzake inadaiwa kuwa walikamatwa na polisi Machi 11, 2017 wakituhumiwa kupanga njama za kuvuruga Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho unafanyika baadaye leo kwenye Kituo cha Mikutano ch Kimataifa cha Dodoma.
Akihojiwa na Televisheni ya Azam, leo Bashe alikataa kabisa kueleza kwa undani kama habari za kukamatwa kwake ni za kweli na kwanini walikamatwa. “Katibu Mkuu atalizungumzia hili, mimi, Joseph Msukuma na Adam Malima, Katibu Mkuu atalizungumza.” Alijibu Bashe.

 Adam Malima
Joseph Kasheku Msukuma
Reactions:

0 comments:

Post a Comment