Friday, 3 March 2017

Hatimaye Mbunge wa Arusha mjiji Godbless Lema amepewa dhamana na Mahakama Kuu mjini humo Leo 3/3/2017. Sharti kuu la dhamana lililotolewa na mahakama hiyo ni wadhamini wawili na bondi ya shilingi milioni 3. Baada ya kuachiwa Lema aliungana na familia yake pamoja na viongozi wa juu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dkt.Mashingi, wajumbe wa kamati kuu, Edward Lowassa na wabunge kadhaa wa chama hicho wakiwemo mamia ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za Ukomboz baada ya mbunge huyo kutoka CHADEMA kukaa miezi 4 mahabusu  baada ya mivutano ya kisheria ya muda mrefu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment