Tuesday, 14 March 2017MENEJA Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu, (SUMATRA), David Mziray, (pichani juu), amefariki mapema alfajiri ya leo Machi 14, 2017 kwenye hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa zilizopatikana mapema leo jijini, ziemseam, mipango ya mazishi imeanza nyumbani kwake Kimara-Temboni jijini Dar es Salaam.
Kwa wana tasnia ya habari watamkumbuka Mziray kwa kuwa karibu na vyombo vya habari kwani pale alipotakiwa kutoa ufafanuzi au maelezo fulani yahusuyo SUMATRA, alikuwa mwepesi kufanya hivyo.
Bwana alitoa Bwana alitwaa na jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu David Mziray peponi. AMIN
Reactions:

0 comments:

Post a Comment