Sunday, 12 March 2017NA K-VIS BLOG, DODOMA
MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi CCM, uliofanyika leo Machi 12, 2017 mjini Dodoma, umepitisha mabadiliko ya 16 ya Katiba yake ya mwaka 1977.
Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kikwete wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa mjini Dodoma, wajumbe kwa kauli moja walihojiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Pombe Magufuli iwapo wanayaafiki mabadiliko hayo au la, na wajumbe waliitikia kuyaafiki.
Katika Mabadiliko hayo, kuanzia sasa, idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho itapungua kutoka idadi ya wajumbe 300 hadi wajumbe 163, huku idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu, (CC), wamepungua kutoka idadi ya wajumbe 34 hadi 24.
Aidha katika mabadiliko hayo, kiongozi wa CCM hataruhusiwa kuwa na vyeo zaidi ya kimoja vya tendaji wa siku hadi siku.
Akizungumzia mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli alisema, “Mabadiliko haya yana lengo la kukifanya chama kijitegemee kiuchumi lakini pia chama ni mali ya wananchi (wanachama) na viongozi ni watumishi tu.”

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. John Magufuli akihutubia mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho
Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Mama Janeth Magufuli akizungumza jambo na mke wa Makamo wa Mwenyekiti wa CCM, (Zanzibar),  Mama Mwema Shein, (kushoto)
 Wake za viongozi
Dkt. Magufuli, akisalimiana na Dkt. Kikwete. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM uliofanyika leo Mkoani Dodoma
  Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Tanga.
 Mama Salma Kikwete, (kushoto), na Waziri Nape Nnauye, ambao ni wajumbe kutoka mkoa wa Lindi


 Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Mara Adam Malima, mjumbe toka mkoa wa Pwani
 Wajumbe kutoka mkoa wa Manyara
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa  katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM uliofanyika leo Mkoani Dodoma
 Khadija Kopa akiwarusha roho wajumbe
 Jukwaa kuu wakishangilia kwa kupeperusha vibendera vya CCM
 Dkt. Magufuli akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, Zubeir Ali Maulid
Reactions:

0 comments:

Post a Comment