Thursday, 2 March 2017Kiungo mchezeshaji wa zamani wa timu ya Liverpool ya Nchini Uingereza, John Barnes akionyesha jezi ya timu ya Taifa kwa waandishi wa habari aliyokabidhiwa na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Machi 2, 2017.


NA K-VIS BLOG
KIUNGO mchezeshaji wa zamani wa timu ya Liverpool ya Nchini Uingereza, John Barnes amewasili Nchini leo Machi 2, 2017 kwa mwaliko wa Benki ya Standard Chartered kuhudhuria fainali za mashindano ya Standard Chartered Road to Anfield ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya benki hiyo yatakayofanyika Jumamosi Machi 4.
Bingwa wa mashindano hayo ya  Standard Chartered Road to Anfield atapata nafasi ya kwenda mjini Liverpool Nchini Uingereza.Timu zilizoingia fainali ya mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.
Sambamba na hilo, Barnes ambaye alikuwa mahiri kwenye eneo la kati akichezea timu hiyo kubwa nchini Uingereza kwenye miaka ya 90, pia atapata fursa ya kutoa mafunzo kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 Serengeti Boys, maafisa wanaoratibu ziara ya mwanandinga huyo wamewaambia waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati akiwasili.


Barnes (wa pili kushoto) akiwa na wenyeji wake, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere- VIP Terminal I Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa pili kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto).


 Barnes akisalimiana na mdau wa soka, Benjamin Thompson Kasenyenda, alipowasili hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam-The Kilimanjaro  
Reactions:

0 comments:

Post a Comment