Thursday, 9 February 2017

 Mwanasheria wa CHADEMA, na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (kushoto), na Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu, (kulia), wakishuka kutoka kwenye karandinga la polisi walipofikishwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Februari 9, 2017, kujibu tuhuma dhidi yao. Watuhuiwa hao ambao wanashtakiwa kwa makosa tofauti wamefanikiwa kuachiwa kwa dhamana.
NA K-VIS BLOG

MISS Tanzania wa zamani, Wema Sepetu na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA wameachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Februari 9, 2017.
Wakati Wema amesomewa shtaka la kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake, Tundu Lissu yeye ameshtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi.
Wema Sepetu amekana shtaka hilo na kupewa dhamana hadi tarehe 20, 2017 kesi yake itakapotajwa tena.
Kwa upande wake, Mwanasheria huyo wa CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, yeye ameshtakiwa kwa kosa la uchochezi ambapo alikiri lakini akasema maneno yake hayakuwa na uchochezi wowote.
Lissu aliachiwa kwa dhamana hadi tarehe 6 Machi, 2017 wakati kesi yake itakapotajwa tena.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment