Thursday, 23 February 2017 MISS Tanzania wa zamani na msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu, (watatu kulia), na mama yake (mwenye kilemba chekundu), wakiwa kwenye benchi moja wameketi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, mahakama kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 23, 2017 ambapo Mbowe anamshitaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi Kanda hiyo, Camilius Wambura. Wema alisema amekuja kumuunga mkono Mbowe katika kesi hiyo

NA K-VIS BLOG
MISS Tanzania wa zaman Wema Sepetu amehamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo Februari 23, 2017 ikiwa ni siku chache baada ya kufunguliwa shtaka moja la kukutwa na Bhangi.
Leo hii Wema ambaye pia ni msanii wa Bongo Movie, akiwa na mama yake mzazi, wamemsindikiza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Mahakama kuu , kusikiliza kesi aliyofungua Mbowe ya kuwashitaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi ,Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam, (ZCO), Camilius Wambura, na mara zote alionekana akionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na upinzani.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, kupitia ukurasa wake wa Facebook, alisema Chama kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Mh.Freeman Mbowe baada ya kusikilizwa kesi ya kikatiba hii leo mahakama kuu atazungumza na Waandishi wa habari kuhusu kupokea wanachama wapya waliojiunga na CHADEMA akiwemo  Wema  Sepetu
Reactions:

0 comments:

Post a Comment