Monday, 13 February 2017


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Sianga, leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Februari 13, 2017.
NA K-VIS BLOG
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya,Rogers Sianga ameanza kazi kwa kishindo…. ni sawa na msemo usemao “upele umepata mkunaji” pale alipoagiza kuwa watumishi wa serikali, wakati huo hadi sasa, ambao kwa namna moja au nyingine waliwezesha kupita kwa vifaa vya “kurutubisha’ dawa za kulevya katika mipaka ya nchi na kuingia nchini, huku wakijua wanatenda kosa, wakamatwe mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa uchunguzi.
Sambamba na hilo, Kamishna huyo ambaye alionekana akiongea kwa upole na kwa uhakika, akionhyesha kubobea kwenye dhamana aliyokabidhiwa hakuishia hapo, ikiwa ni ndani ya saa 24 tangu kuapishwa kwake, tayari yeye na timu yake, wameanza kuyapitia mafaili ya hukumu zote za kesi zinazohusiana na dawa za kulevya ambazo kwa maoni yake “zilivurugwa” kwa makusudi na hivyo watuhumiwa kuachiwa huru.
“Mtu anaingiza kilo hamsini za madawa, Jaji anasema namuachia huyu hana hatia.” alisema
“Tunayo orodha ya mahakimu, majaji na wanasheria wa serikali, tutaipeleka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, ili wachunguzwe na ikionekana walikiuka sheria nao waondolewe kwenye nyadhifa zao.
Akizungungumza kutoka ukumbi mku bwa wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Februari 13, 2017 katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamishna Mkuu huyo aliapa, kuwa katika vita hii hakuna atakayepona lazima wote wafikiwe na mkono wa sheria.
Akitumia msemo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wa “Jiwe litasaga jiwe na kuwa unga”, akimaanisha vita hii dhidi ya dawa za kulevya haina cha msalie mtume, na kwamba, hata wale “PAPA” ambao walikuwa hawashikiki nao wakashukiwa na Mamlaka yake.
Akitaja uhalifu wa dawa za kulevya, Kamishna huyo alisema, uko katika makundi matatu, moja likiwa wasafirishaji, watumiaji na wafadhili na kwamba wote hao wanaangukia katika “kapu moja”.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, alimkabidhi kamishna huyo orodha ya majina ya watu zaidi ya 90 ambao alisema ni wale “nyangumi” yaani wauzaji wakubwa, hata hivyo hakuwataja.
Makonda aisema orodha hiyo imesheheni majina ya wanaotuhumiwa kuuza, wanaosambaza, wanaotumia, wanaofadhili na kuwezesha tangu serikali ya awamu ya pili, ya tatu ya nne na walioanza kwenye awamu hii ya tano.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa. RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya pili iliyoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kuendelea mpaka awamu ya sasa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohammed almaarufu TID akitoa ushuhuda wa namna alivyokuwa akitumia Dawa za kulevya,na sasa amekiri hadharani kuacha kutumia na kuunga mkono juhudi za kupambana na Dawa za kulevya.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo, ambapo amekabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William sianga ili yaanze kushughulikiwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya, Rogers Sianga, (kulia), akinong'onezana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Februari 13, 2017 wakati wa kikao cha wadau kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Reactions:

0 comments:

Post a Comment