Saturday, 18 February 2017


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kudhibioti na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga.(PICHA YA MAKTABA)

NA K-VIS BLOG
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuapmbana na Dawa za kulevya, Rogers Sianga, amesema uchunguzi wao hadi sasa hawajaona uhusika wa moja kwa moja wa wanasiasa hapa nchini kwenye biashara ya dawa za kulevya.
“Bahati nzuri unaposhughulika na dawa za kulevya watu hawa hawajifichi, tabia zao, mienendo yao na maisha yao hayajifichi, kwa kiasi kikubwa wanasiasa hatuoni connection ya uhusika wao, lakini siwezi kusema kwamba hakuna watu wa aina hii wanaohusika, lakini huko tuendako, yawezekana tukawajua hawa yawezekana atakayekamatwa ni jamaa yake, mtoto wake au ndugu yake.
Akizungumza asubuhi hii ya leo Jumapili Februari 19, 2017 na mtangazaji Tido Mhando kwenye kipindi cha Funguka, Kamishna Mkuu Sianga pia amesema Tanzania wapo Wafanyabiashara wakubwa kingpin wawili wa kuuza dawa za kulevya wanaotambulika kimataifa, mmoja yuko gereza la Segerea alikamatwa tarehe 31/6/ 2010 ambaye ni mwanamama.
Mwana mama huyu huko jimbo la Hanova nchini Ujerumani ana kesi 40 za watu aliowatuma kufanya biashara hiyo ya dawa za kulevya.
Mtu wa pili ni mwanaume yuko kwenye gereza moja hapa nchini, alitajwa kuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya, Marekani Ulaya, Afrika na Australia wamemtaja kuwa wanamtafuta.
Huyu alikuwa na nguvu ya kuagiza dawa za kulevya kwenye viwanda vinavyozalisha akielekeza kiwango cha Purity ya dawa anazohitaji, mathalan 7% ya kiwango cha level ya purity ni Mtanzania.
Pia amezungumzia suala la Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kupelekwa mahakamani kwa kosa la kutumia dawa za kulevya.

“Watuamiaji wa dawa za kulevya tunawakamata kama vyanzo vyetu vya habari, ili kujua ni wapi wanapata hayo madawa, nay eye hatyumuachi, tunampeleka kwenye rehab ili apate matibabu, kwa wale wanaokataa, tunamuweka kwa siku mbili tatu ili ile AROSTO impate na hatimaye atataja tu.” Alisema.
Kwa wale ambao wameshiriki vizuri, hatuwapeleki mahakamani, sisi tunachokifanya ni kumsaidia ili kumuondoa kwenye uraibu”.
Hayo ameyasema, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, Rogers Sianga, wakati akiongea na Mtangazaji Tido Mhando kwenye kipindi cha Funguka kinachopeperushwa na Televisheni ya Azam Tv ya jijini Dar es Salaam.
Pia Kamishna Sianga amesema, katika kipindi uchunguzi wao hadi hivi sasa, bado hawajaona uhusika wa moja kwa moja wa wanasiasa katika biashara ya dawa za kulevya.
Kamishna Rogers pia alisema, Mtanzania mwingine alikamatwa 2014 lakini hajatangazwa kama kingpin lakini ana nguvu kubwa na yuko gerezani.
Pia wako wengine kadhaa wakubwa wako kwenye magerezani mbalimbali ambao wametetemesha bara la la Afrika, amesema Kamishna Sianga.
“Suala la kufanya biashara ya madawa ya kulevya , muundo ule unaotumika kusafirisha dawa hizo sio wa kudumu, ukiondoa vingozi wa juu uliowakamata, inaundwa nhingine na hakuna kinachosimama na hakuna kinachodumu it’s never permanent inanyumbuka kila wakati, kwa hivyo kazi yetu ni mpekecho tunaendelea kupambana nao.
 “Katika jambo lolote political will ni jambo muhimu sana, inakusaidia wewe mtendaji kujijua je niko salama, hata ukiwa unashughulika na hao vigogo unakuwa huna wasiwasi, unakuwa na ari ya kufanya kazi.” Alisema.
“Sekeseke la kupambana na dawa za kulevya linahitaji nguvu, diplomasia haina nafasi sana, kinachobadilisha ni mbinu au taratibu za hatua tunazochukua, mapambano ni yale yale, tumepokea orodha, kila jina tulilopewa tunakwenda nalo, watu hivi sasa wako mtaani, tayari tunaye mtu mkubwa tu tumemkamata asubuhi ya leo, na tunaanza kukusanya maelezo yake.
“Lakini tunajaribu kuwa makini na taarifa tunazopata, kwani inawezekana mtu akataja jina la mtu kwa chuki, na hivyo tukajikuta tunaingia kwenye matatizo makubwa.” Alisema.
Tunatumia neon “JAPAN” katika kufanyabkazi zetu, neon hili Japan halimaanishi nchi ya Ujapan, la hasha, hili neon linatumika katika shughuli zetu hizi na maana yake ni hii J ni-, Justify, (Sababu), Authority(Mamlaka kisheria), Proportional (nguvu unayotumia), Admini (Utawala), Necessity( Umuhimu).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment