Tuesday, 28 February 2017

 Hii ndiyo transfoma kubwa iliyolipuka huko Buguruni  jijini Dar es Salaam
 Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuutaarifu umma kuwa Jumapili ya tarehe 26/02/2017 majira ya saa kumi alasiri kulitokea moto katika chumba cha transfoma kubwa iliyopo eneo la Tazara (Buguruni Substation) na kusababisha kuungua kwa Transforma kubwa ya Buguruni (15mva, 33/11kv) na hivyo kusababisha  maeneo ya Vingunguti, Kiwalani, Baadhi ya viwanda viliyopo barabara ya Nyerere na maeneo yaliyo jirani na haya kukosa Umeme. Kazi bado inaendelea na pindi itakapokamilika Umeme utarejea katika hali yake ya kawaida. Baada ya kutokea kwa moto huo jitihada za kuuzima zilianza ikiwa ni pamoja na kuwapigia simu "fire" ambao walifanikiwa kuuzima moto huo ambao ulikuwa umeshaharibu transforma hiyo kwa kiasi kikubwa. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wote unaoendelea kujitokeza.Reactions:

0 comments:

Post a Comment