Thursday, 9 February 2017


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Usimamizi ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), imefanya kikao kazi na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania, (TUCTA), jijini Dar es Salaam Februari 9, 2017 na kuhimiza ushirikiano mpya ili kuwatumikia wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi.
Akitoa mada kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, (pichani juu), alisema, SSRA ni Mamlaka ya serikali yenye wajibu mkubwa wa kulinda maslahi ya wafanyakazi.
“Leo hii naomba niwe msikilizaji zaidi ili ninyi wanachama wa TUCTA ambao mnawakilisha wanachama wa Mifuko mbalimbali hapa nchini, muweze kuelezea namna nzuri ya kuwahudumia wanachama wetu, na ndio maana tumeona tuitishe kikao hiki ili kusikiliza kutoka kwenu.” Alisema Bi. Isaka.
Akielezea mambo ambayo SSRA inasimamia ni pamoja na kuhakikisha Mifuko inatimiza wajibu wake katika kuwatumikia wanachama wake.
Alisema kazi za SSRA zimeanishwa chini ya Kifungu 5(1), cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, na kazi hizo ni pamoja na kusajili Mifuko, watunzaji na meneja wa uwekezaji wa sekta ya hifadhi ya jamii, kutoa miongozo kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii lakini kubwa zaidi ni kutetea na kulinda maslahi ya wanachama.
Bi Isaka alitoa wito kwa uongozi wa TUCTA kujenga ushirikiano wa karibu na kusaidia SSRA katika kutoa elimu kwa wanachama pamoja na waajiri juu ya wajibu wao katika kuchangia Mifuko na hatimaye kusaidia utoaji wa huduma kuwa rahisi na haraka.
Kwa upande wake, Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamuhoka, aliishukuru SSRA kwa kuwaita wawakilishi wa vyama 13 vya wafanyakazi nchini, ili kusikia kutoka kwao nini changamoto zinazowakabili wanachama wao katika eneo hili la hifadhi ya jamii.

 Bi. Irine Isaka, akitoa mada kwenye kikao hicho
 Bi Isaka akisalimiana na wajumbe wa kikao hicho kabla hakijaanza
 Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamuhoka,akizungumza wakati wa kikao hicho
  Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamuhoka,akizungumza wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Bi. Irine Isaka
 Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kikiendela kwenye kikao
 Mkurugenzi wa Huduma nna Sheria wa SSRA, Bw. Onorius Njole, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza.
 Mkurugenzi wa Tathmini na Sera , SSRA, Ansgar Mushi, akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Viongozi wa SSRAwakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikizungumzwa
 Makuu wa mawasiliano ya umma na uhamasishaji, Bi. Sara Kibonde Msika (kushoto), akizungumza wakati wa kikao hicho
 Mmoja wa wajumbe, Dkt.Francis Michael, akizunumza wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya TUCTA, Bi. Leila Bhanji, akiuliza maswali juu ya fao la uzazi.
 Katibu Mkuu wa TUCTA, Dkt. Yahya Msigwa, (kushoto), akizunhguzma jambo huku Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka na Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamuhokya wakisikiliza
 Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamuhokya wakisikiliza
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akitoa shukrani kwa wajumbe
 Baadhi ya wajumbe wakijadiliana
 Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, uongozi wa TUCTA na wanachama wa TUCTA
Uongozi wa TUCTA katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa SSRA
Reactions:

0 comments:

Post a Comment