Saturday, 25 February 2017
NA K-VIS BLOG
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, ikicheza pungufu kwa muda mrefu wa kipindi cha pili, imeidhalilisha Yanga kwa kuichapa mabao 2-1 katika pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao mawili ya Simba yalifungwa na Lodit Mavugo, katika dakika ya 60 kwa mpira wa kichwa baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa na winga aliyeingia kipindi cha pili Shiza Kichuya.
Katika dakika ya 81, Shiza Kichuya akiwa nje ya “boks” alifumua shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Yanga Deogratius Munisi “Dida” na kuandika bao la pili.
Bao la Yanga lilifungwa kwa njia ya penati katika dakika ya 4 na mshambuliaji Simon Msuva kwa njia ya penati baada ya mlinzi wa Simba Novert Lufunga kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga Chirwa ndani ya eneo la hatari. Simba inaendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kujikusanyia jumla ya pointi 54 mbele ya Yanga yenye pointi 49.
Mlinzi wa Simba Mkongomani Lukungu, alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment