Friday, 24 February 2017


NA K-VIS BLOG
MBUNGE wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (pichani), amesema anatamani katika safari yake ya kisiasa hapo baadaye awe Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ridhwani ameyasema hayo asubuhi hii Februari 25, 2017 wakati akijibu swali la mtangazaji wa kipindi cha runinga cha asubuhi cha televisheni ya Clouds 360 on Saturday.
“Nini political ambition yako, je unatamani siku moja uwe Rais wa nchi hii? Aliulizwa Ridhwani na mtangazaji huyo, naye akajibu. “Mimi sitamani kuwa Rais, lakini  natamani sana siku moja niwe Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.” Alijibu Ridhwani, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Hata hivyo Ridhiwani amabye alialikwa kwenye kipindi hicho kuelezea mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jimbo lake la Chalinze, alisema, nia yake hiyo sio kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya Kinana.
“Hapana sifikirii kuwa Katibu Mkuu baada ya Kinana, wazo hili ni hapo baadaye siyo wakati huu.” Alijibu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli, (kulia), akiteta jambo na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, hii ilikuwa mwaka 2015 wakati wa mikutano ya kampeni huko Chalinze. (Picha ya Maktaba)
Ridhwani Kikwete, (kulia), akitambulishwa na baba yake, Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, kwa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kiongozi huyo wa Marekani hapa nchini. (Picha ya Maktaba)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment