Monday, 6 February 2017

 AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Pombe Magufuli, amemuapisha Mkuu wa Majeshi, (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na kuonya kuwa vita dhidi ya madawa ya kulevya siyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pekee na kuvitaka vyombo vyote vya ulinzi na usalama, kuingia kazini na kuhakikisha hakuna "atakayepona".
Rais amesema hayo katika hotuba yake aliyoitoa muda mfupi baada ya zoezi hilo la viapo lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Februari 6, 2017.
"Katika vita hii ya madawa ya kulevya, hakuna cha mtu aliyemaarufu, hakuna mwanasiasa, hakuna askari, hakuna waziri au mtoto wa fulani ambaye akijihusisha aachwe, hata angekluwa mke wangu hapa Janet wewe shika tu, kwa sababu madawa haya ya kulevya kwa taifa letu hili sasahivi yamefikia mahala pabaya, haiwezekani watu wawe wanayauza kama njugu, si siri, sisi wote tuliopo hapa tunafahamu madawa ya kulevya yanapoteza nguvu kazi ya watanzania wengi na hasa vijana. Kwa hivyo nawaagiza vyombo vyotye, jeshi la polisi na wengine wote wanaohusika endeleeni kufanya kazi zenu, hii siyo kazi ya Makonda ni ya watanzania wote, shika yoyote peleka mahakamani, na ndiyo maana nawaeleza hakuna cha umaarufu, mkishika hawa wote wanaovuta madawa ya kulevya wote, watawaeleza nani aliyewauzia, na huyo aliyewauzia mkimshika ataeleza ameyapata wapi, na huyo mliyemshika atawaeleza ameyapata wapi, lazima mtengeneza hiyo chain yote ya kuhakikisha wanaohusika na madawa ya kulevya wanashughulikiwa kikamilifu." Alifafanua Rais Magufuli katika hotuba yake.
Wengine waliokula kiapo ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, (Chief of Staff), Luteni Jenerali, James Alois Mwakibolwa. Habari kamili inapatikana hapo chini.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venence Salvatory Mabeyo, akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, Februari 6, 2017. (PICHA NA IKULU) 
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali, James Alois Mwakibolwa, akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, Februari 6, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Jenerali kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Jenerali Juma Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Nyakimura Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wakwanza kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wapili kulia pamoja na Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza mara baada ya tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania pamoja na  Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (watatu kutoka kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanne kutoka (kulia) , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (wakwanza kushoto), Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo(watatu kutoka kulia ), Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Luteni Jenerali James Mwakibolwa (wapili kutoka kushoto),  Kamishna Jenerali wa Magereza Juma Malewa(wapili kutoka kulia) pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma(wakwanza kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP) Ernest Mangu mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment