Friday, 17 February 2017


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akimfafanulia sheria mbalimbali ambazo mfanyabishara wa kazi za filamu na muziki anastahiki kuzifuata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo. Anaemsikiliaza Mheshimiwa Nape ni mmiliki wa ghala ambalo shehena kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki zimekamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika leo eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.


Fundi wa kuchoma vyuma kwa kutumia teknolojia ya gesi akiendelea na zoezi la kuchoma kufuli ya lango la ghala lililofichwa kwenye hoteli ya Butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda eneo la Kariakoo. Ghala hilo limekutwa na shehena kubwa ya kazi haramu za muziki na filamu.(P ICHA NA MAELEZO)


Mmiliki wa ghala lilolokutwa chini ya hoteli ya Butterfly Phili Ulaya akijaribu kujitetea mbele za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye mara baada ya zoezi la kuvunja kufuli ya lango la ghala hilo kukamilika. Waziri Nape kwa kushirikiana na viongozi wa taasisi zinazosimamia maslahi ya kazi za ubunifu wamefanya operesheni iliyofanikisha kukamtwa kwa  shehema kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki kwenye ghala la bwana Ulaya liliofichwa chini ya hoteli ya Butterfly.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Filamu wa Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo wakati wa operesheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa shehena kubwa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikagua rundo la filamu zilizokamatwa kwenye opersheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Kwenye operesheni hiyo shehena kubwa ya kazi za filamu na muziki imekamatwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya Butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo jijini Dar-es-salaam.Jengo la hoteli ya butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda, Kariakoo ambalo ghala lenye shehena kubwa ya kazi za haramu za filamu na muziki zilikamatwa kwenye zoezi lililoongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment