Friday, 17 February 2017

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, (kushoto), akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, muda mfupi kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hajazindua baraza la Udhibiti Dawa za Kulevya jijini Dar es Salaam, leo Februari 17, 2017.
NA K-VIS BLOG
MAMLAKA ya Udhibiti dawa za kulevya imewatia mbaroni maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), kwa tuhuma za kusaidia kuingizwa kwa tani 22 za kemikali zinazosaidia kutengeneza dawa za kulevya aina ya Hereon, (Precursor chemical).
Kamanda wa operesheni wa Mamlaka hiyo, Kamishna, Mihayo Msekela amesema, maafisa wengine bado wanahojiwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote.
“Uingizaji mizigo unashirikisha idara nyingi za serikali, na kwa sasa tunawashikilia maafisa wawili wa idara ya Mapato TRA, kwa kusaidia kuingizwa kwa kemikali hizo ambazo hutumika kutenegenza heroin.” Alifafanua Kamanda Mihayo, kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo, Upanga jijini Dar es Salaam leo Februari 17, 2017.
Wakati Mamlaka hiyo ikitangaza hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa a,mbaye ndiye mwenyekiti wa baraza la kupambana na dawa za kulevya, amelizindua baraza hilo jijini Dar es Salaam, leo Februari 17, 2017 na kuwataka wajumbe wa baraza hilo ambao ni mawaziri wa baadhi ya wizara kutoka bara na visiwani, wakuu wote wa mikoa, na wakuu wa vyombo vyombo vya ulinzi na usalama kutoikaribia rushwa katika mapambano haya ambayo aliyaita kuwa ni makuno.


 Waziri Mkuu Kassim majaliwa, akizindua baraza hilo leo
 Kamishna Mkuu Sianga akijitambulisha
 Waziri wa Mabo ya Nje, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (katikati), Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, akizungumza. (PICHA NA MAELEZO)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment