Monday, 20 February 2017
NA K-VIS BLOG/NA MASHIRIKA YA HABARI
BALOZI wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa, (UN), Vitaly Churkin, (pichani katikati), amefariki dunia baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake.
Taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa zinasema, Balozi huyo “gwiji” wa Diplomasia, alifariki baada ya kujisikia vibaya (kuumwa), akiwa ofisini kwake kwenye majengo ya UN, Februari 20, 2017 na tayari Rais wan chi hiyo Vladimir Putin, amesikitishwa na kifo hicho na kumuelezea balozi huyo kuwa ni mtu makini.
Baada ya kuugua ghafla, alipelekwa hospitali, ambako alifariki wakati akitibiwa ingawa sababu hasa za kifo chake hazijajulikana, Naibu Balozi wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Vladimir Safronkov amethibitisha.
Churkin amekuwa balozi wa Russia kwenye Umoja wa Matifa tangu mwaka 2006 na ndiye balozi aliyedumo kwa miongo na lidhaniwa kuwa ndio Balozi mwenye nguvu sana wa Russia ambapo alifanya kazi kwa muda mrefu kwenye chombvo ikubwa cha Baraza la Usalama.
Huyo ni balozi wa pili wa Russia kufia akiwa kazini, Desemba 20, 2016, Balozi Andrei Karlov wa Russia nchini Uturuki, aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Ankara na afisa wa polisi aliyejifanya kuwa mlinzi wake.
Muuaji alikuwa kipiga kelele “Usisahau Alepo, usisahau Alepo”, wakati akifyatua risasi.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment