Monday, 27 February 2017


Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
 Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.
 
Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.

“Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.

Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.

Kabati alisema kuwa ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.

“Hivi  hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema Kabati

Aidha Kabati alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais wetu.

Naye Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.

Mtove aliongeza kuwa atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata hiyo.

“Angalia hadi saizi tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment