Saturday, 18 February 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa hafla ya utoaji wa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la Ulinzi waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.(PICHA ZOTE NA IKULU/MAELEZO).

Maofisa wapya wa Jeshi la Ulinzi Tanzania wakivalishana vyeo mara baada ya kupewa Kamisheni na Rais John Pombe Magufuli katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akitoa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la Ulinzi Tanzania waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22. Katika wahitimu wa jumla walikuwa 180 ambapo 15 ni kutoka nchi jirani za Uganda(2), Burundi(5), Rwanda(3) na Kenya(5).
Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya  Chaso ya Pemba wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotunuku  Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Maofisa wapya wa Jeshi la Ulinzi Tanznia mara baada ya kumalizika kwa zoezi la utoaji wa Kamisheni kwa Maofisa ha oleo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Kwanza Jenerali Mstaafu Merisho Sarakikya, Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya zoezi la kutoa Kamisheni kwa Maofisa wa Jeshi la Ulinzi waliohitimu Chuo cha Mafunzo kwa Maofisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha, leo Jijini Dar es Salaam. Takribani Maofisa 165 wamepewa Kamisheni kati yao Wanaume ni 143 na wanawake ni 22.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment