Monday, 23 January 2017


 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
TANZANIA na Uturuki zimetiliana saini mikataba tisa (9), ya ushirikiano katika nyanja za ulinzi, biashara, afya, elimu, habari na utalii.
Mikataba hiyo imesainiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, na mawaziri wa kisekta wa mataifa hayo mawili mbele ya Rais John Pombe Magufuli na mgeni wake, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Rais Erdogan yuko nchini kwa ziara ya siku mbili ikiwa nis ehemu ya ziara yake ya kutembelea mataifa matatu ya Afrika, mengine yakiwa ni Msumbiji na Madagascar.
Rais huyo ambaye amefuatana na mawaziri waandamizi wa serikali yake na wafanyabiashara wanaokadiria kufikia 100, alifanyiwa sherehe za kidola kwenye viwanja vya Ikulu, ambapo baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Magufuli, Rais huyo wa Uturuki alipigiwa mizinga 21 ikiwa ni ishara ya heshima kwa kiongozi wa taifa anayetembelea Tanzania.
Baada ya kupoigiwa mizinga hiyo, Rais Erdogan alikagua gwaride la kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, kabla ya kuongozana na mwenyeji wake kuelekea ukumbi wa mikutano wa Ikulu ambapo awali marais hao wawili walibadilishana zawadi, kabla ya kufanya mazungumzo rasmi, yaliyofuatiwa na sherehe za utiwaji saini mikataba hiyo.
na kufuatiwa na hotuba za viongozi hao wawili ikianza hotuba ya Rais Magufuli na kufuatiwa na ile ya mgeni wake. Pichani juu Marais hao wawili wakishuhudia mawaziri wao wakiweka saini mikataba hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 23, 2017. 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment