Thursday, 19 January 2017

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (kuli), akipokea na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abassi, alipotembelea Idara hiyo jijini Dar es Salaam, Januari 19, 2017 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. (PICHA NA FRANK SHIJA-MAELEZO)
 Waziri Nape, akipatiwa maelezo na Dkt. Abassi na maafisa wengine wa idara ya Habari Maelezo kuhusu ukumbi unaotumika kwa mikutano na waandishi wa habari
Afisa Habari Mkuuwa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. John Lukuwi akimuelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye( aliyekaa) namna Kamera ya kupiga picha majengo marefu inavyofanya kazi.
 Waziri Nape, akionyeshwa habari zilizochapishwa na moja ya magazeti nchini miaka ya nyuma, wakati waziri Nape alipotembelea maktaba ya Idara hiyo
 Waziri Nape, akipitia baadhi ya magazeti yaliyochapisha habari miaka ya nyuma, wakati alipotembelea maktaba ya Idara hiyo.
 Waziri Nape akiwa katika moja ya maktaba za Idara ya Habari Maelezo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Bw. Vincent Tiganya.
 Waziri Nape, akionyeshwa saver ya kutunza picha ya Idara ya Habari Maelezo. Kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Idara hiyo, Bw. John Lukuwi.
Picha ya pamoja
Reactions:

0 comments:

Post a Comment