Sunday, 29 January 2017


WACHIMBAJI 15 wa madini waliofukiwa na kifusi siku tatu zilizopita kwenye mgodi unaomilikiwa na kampuni ya RZ huko Nyarugusu, mkoani Geita, hatimaye wameokolewa wakiwa hai.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia kutoka mkoani Geita, wachimbaji hao wameokolewa ikiwa ni ndani ya masaa 24 tangu walipojibu ujumbe uliotumwa kwao, na wao wakajibu wako hai na wanachohitaji ni kupelekewa chakula,
Taarifa zinasema, mchimbaji wa kwanza alkokolewa majira ya saa tatu asubuhi hii ya Januari 29, 2017 na kufuatiwa na wenzake.Walionekana wakiwa wamejaa tope lakini wakiwa na afya njema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment