Saturday, 14 January 2017


NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Angelina Mabulla  ameagiza Idara za Ardhi katika Halmashauri nchini  kutoa ramani za makazi kwa wenyeviti  wa mitaa na vitongoji ili  kujua maeneo yao na kupunguza migogoro ya ardhi  ambayo inasababisha baadhi ya wananchi kuvamia maeneo  bila kujua  maeneo hayo yametengwa kwa matumizi mbalimbali. Akizungumza na watumishi   wa manispaa ya Songea  jana, ameagiza hadi kufikia Machi mwaka huu ramani zote za makazi ziwe zimefika kwa wenyeviti wote na kusisitiza kuwa alama zote zilizopo  katika ramani hizo zifafanuliwe na kueleweka  kwa wenyeviti  hao.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment