Sunday, 15 January 2017

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA  (TANESCO)

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha vikali Taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Umeme ulioingizwa katika mita ulisababisha mita kulipuka na kumjeruhi Mteja.

Tungependa Umma ufahamu kuwa huu ni uzushi wenye nia moja tu ya kuchafua taswira ya Shirika.

Umeme unaonunuliwa kwenye Simu ni sawa na Umeme unaonunuliwa katika vituo vyote vinavyouza Umeme na hakuna uhusiano wowote wa kitaalamu au kihandisi unaoweza kusababisha Umeme unaoingizwa kutoka kwenye Simu kusababisha Mita kulipuka.

Tunawaomba wateja wetu  kuendelea kutumia huduma zetu bila hofu na kuipuuza taarifa hiyo ya uzushi.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano 
TANESCO Makao Makuu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment