Thursday, 26 January 2017

 Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (kulia), akimkabidhi tuzo, Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Sara Kibonde Msika, kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Januari 26, 2017. Mamlaka hiyo na ile ya Mapato, TRA zilikabidhiwa tuzo za ubunifu na Umoja wa Afrika hivi karibuni.
  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (kulia), akimkabidhi cheti Meneja wa Customs Automation wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Tinkasimile Felix.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), zimetunukiwa tuzo za ubunifu katika utoaji huduma na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Akikabidhi tuzo hizo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Msemaji wa wizara hiyo, Bi Mindi Kasiga, (pichani juu),  alisema Umoja wa Afrika umezitunuku Mamlaka hizo mbnili kutokana na ubunifu katika utoaji huduma.
Akizunhgumzia tuzo ambazo SSRA imekabidhiwa, Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka hiyo, Bi. Sara Kibonde Msika alisema, kupitia wataalamu wa nje na ndani Mamlaka ilibuni mfumo mtambuka ya kupanua wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa kutumia Tehama, ambapo ilianzisha mradi wa Kanzi Data ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii (National Social Security Collaborative Database Bridge (NSSCDB).
Alisema takwimu za Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini kwa kipindi kinachoishia Juni 2016, Mifuko yote nchini ina jumla ya wanachama Milioni 2.46.
Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Nchini, (TRA), Bw. Richard Kayombio alisema, TRA imekuwa ikiboresha huduma zake katika miaka ya hivi karibuni ambapo utoaji wa huduma katika Mamlaka hiyo umekuwa ni wa haraka na wenye manufaa makubwa.
Alisema, kwa kiasi kikubwa TRA imekuwa ikitoa huduma zake kwa kutumia Tehama na hivyo kupunguza usumbufu na muda mwingi uliokuwa ukitumiwa na wateja katika kufanya malipo mbalimbali.

 Mkurugenzi wa Uhusiano Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Nchini, (TRA), Bw. Richard Kayombio
 Picha ya pamoja kati ya msemaji wa wizara, na maafisa wake na watunukiwa
 Picha ya pamoja, msemaji wa wizara na watunukiwa wa TRA
Bi. Mindi Kasiga, (kushoto), akimkabidhi cheti, Bi. Sara Kibonde Msika
Reactions:

0 comments:

Post a Comment