Friday, 6 January 2017


NA K-VIS BLOG, Karagwe
SOKO kuu  la Kayanga, wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Januari 7, 2017.
Hii ni mara ya pili kwa soko hilo kuteketea kwa moto, wakati chanzo cha moto uliotokea mara ya kwanza Aprili 2016, kilikuwa ni jiko la mkaa, chanzo cha moto huu wa sasa, bado hakijajulikana, Mbunge wa jimbo la Karagwe, Bw. Innocent Bashungwa, amethibitisha.
“Bado moto unaendelea hivi sasa (asubuhi), lakini tunashukuru hakuna maafa ila mali za wananchi zimeteketea, wananchi wanalia, tumepata msada wa gari la zimamoto, limejitahidi kuzima moto ule mkubwa.” Alisema Mbunge huyo.
Hii imekuwa balaa, baada ya balaa, tumepata tetemeko, tukapambana serikali imesaidia inavyoweza, tumepata balaa la ukame, bado tunaendelea nalo, na sasa balaa la moto, wananchi wamechukua mikopo, sasa sijui watalipaje.” Alisema Mbunge huyo wakati wa mahiojiano ya moja kwa moja na Radio One Sterio mapema leo asubuhi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment