Thursday, 12 January 2017NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ataitembelea Tanzania, Januari 22-23 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne ya kutembelea mataifa matatu ya Afrika.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Nchi hiyo, Andolu, ziara ya kiongozi huyo itaanzia Tanzania, kabla ya kuendelea na mataifa ya Msumbiji, na Madagascar.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa mataifa ya Kiafrika na Uturuki. “Kukua kwa ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika, kunaonyesha mengi yanaweza kukamilishwa kwa kuhusisha washirika kwa nia njema na kutafuta ufumbuzi wa kimaslahi wa pande mbili” Alisema Erdogan wakati wa ziara kama hii aliyoifanya barani Afrika Juni 2016.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment