Thursday, 19 January 2017


NA K-VIS MEDIA/MASHIRIKA YA HABARI
WASAIDIZI wakuu wa Rais Yahya Jammeh wa Gambia, waanza kumkimbia, ikiwa ni saa chache kabla ya Rais mteule wa nchi hiyo, Adama Barrow, kula kiapo jioni hii kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Kiongozi wa juu kabisa kumtoroka “Bosi” wake ni Makamu wa Rais, Isatou Njie Saidy na Mwanasheria wake Edu Gomez .
Taarifa ya vyombo vya habari vya kimataifa iliyotolewa leo Januari 19, 2018, inasema, vikosi vya jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, (ECOWAS), tayari vinajiandaa kuivamia Gambia, ikiwa kiongozi huyo atang’ang’ania kuwa madarakani.
“Ikiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Gambia, atahitaji msaada wa kijeshi, majeshi ya ECOWAS yako tayari kufanya hivyo,” Msemaji wa Serikali ya Nigeria aliiambia BBC.
Bw. Barrow ambaye alishinda kiti cha Rais wa Gambia mwezi uliopita, amekimblia nchini Senegal kwa usalama wake, na ameandika katika akaunti yake ya Tweete akisema, ataapishwa leo Alhamisi Januari 19, 2017 kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
Vikosi vya ECOWAS vikiongozwa na Senegal tayari viko mpakani vikisubiri amri kuvuka mpaka.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Gambia, Sidi Sanneh, amesema, kuna mgawanyiko katika jeshi la Gambia, wakati Mmkuu wa Majeshi tayari ameshatangaza kuwa vikosi vyake havitajiingiza katika vita ya kijinga, lakini kuna kundi dogo la wanajeshi linalofaidi zaidi linaweza kuleta upinzani.
Rais Yahya Jammeh, akiwa na umri wa miaka 29 mwenye cheo cha Luteni, aliongoza kikundi cha wanajeshi na kumpindua Rais aliyekuwa madarakani wakati huo, Dawda Jawara, Julai 22, 1994. Mapinduzi hayo hayakuwa na umwagaji damu.
Naye Dawda Jawara aliitawala nchi hiyo tangu mwaka 1970.

Rais wa Gambia aliyepinduliwa na Jammeh, Bw. Dawda Jawara
Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow
Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Njie Saidy.
Mwanasheria wa Rais Jammeh, Edu Gomez .
Reactions:

0 comments:

Post a Comment